1. Pombe za Chimpumu, Dengerua,
Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku.
Hupoteza uwezo wa kufikili wa mtumiaji Huongeza ufanisi wa viungo vya mwili
vilivyo katikati ya miguu ya mtumiaji chini ya kiuno kwa mbele, hivyo kuongeza
uwezekano wa mtumiaji kujiusisha na ngono zisizo salama na kubaka. Zaidi ya 60%
ya kesi zote za kubaka zilizotokana na ulevi zimehusishwa na utumiaji wa pombe
hizi!Hukakamaza misuli ya midomo na kuongeza ufanisi wa koromeo
(voicebox),hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakipayuka ovyo na
kwa sauti za juu kuliko kawaida.
2. Pombe za Pingu na Gongo
Hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa
kufikiri wa mtumiaji Huongeza joto la mwili la mtumiaji kwa kuongeza spidi ya
metabolism (metabolic activities), hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuvua
nguo hadharani, ili kupunguza joto la mwili! Kwa upande wa pombe ya pingu, hii
huongeza spidi ya myeyusho wa chakula(Digestion) na ikitokea mtumiaji hajala
kwa muda mrefu huishia kutapika mpaka nyongo. Baada ya kuongeza spidi ya
myeyusho wa chakula pombe hii hulegeza vifuniko vya mwili (sphincter muscles)
hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuachia kokoo madimba iliyo rojorojo(uharo
wa nguvu na wenye harufu kali). Kwa watumiaji wa lile gongo litengenezwalo kwa
kinyesi cha binadamu (kigamboni ni eneo maarufu kwa biashara hii), wengi wao
huishia Intensive Care Units (ICU), na baada ya hapo hupelekwa Psychiatric
Units (wodi za vichaa), kwani zaidi ya 63% ya watumiaji wa pombe hii huishia
kuwa vichaa kamili!
3. Pombe ya Mnazi
Kiasi cha ulevi (alcoholic contents) kilichomo katika pombe hii,hushambulia
sehemu ya ubongo wa kati (cerebellum), ihusikayo na kutunza utashi, hivyo si
ajabu kwa mtumiaji wa pombe hii kuishia kuvurumusha matusi ovyo na kuyumba
barabara nzima!Iwapo mtumiaji wa pombe hii hatakuwa mwangalifu na hivyo kunywa
mdudu fulani aitwaye kigoto anayekuwa katika pombe hii, basi mtumiaji huyo
atakuwa mlevi mbwa wa mnazi maishani mwake!Watu hushauriwa kuviepuka vyoo
vilivyotumiwa na walevi wa pombe hii kwani harufu wanayoiacha huko chooni
inahusishwa na kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya pua na ubongo (nose and cerebral
cancer)
4. Pombe ya Ulanzi
Pombe hii hushambulia viunganishi vya
mwili (Body Joints), kwa hiyo asilimia kubwa ya watumiaji wa pombe hii huishia
kulala mabarabarani,vyooni na sehemu nyingine zisizo za kawaida kwa kushindwa
kutembea!
5. Pombe za Bia, Konyagi. Wiski na Wine mbalimbali
Pombe hizi huongeza hali ya kujiamini kwa watumiaji na pia kuwakumbusha kuwa
hapo zamani za kale, waliwahi kupitia shule,hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji
wa pombe hizi wakizoza kimombo na kujihusisha na mijadala isiyo na kichwa wala
miguu punde baada ya kulewa!Pombe hizi hushambulia sehemu zilizo katikati ya
miguu chini ya kitovu kwa mbele ya mtumiaji na kuzifanya sehemu hizo kuwa imara
na zenye nguvu(strong and active) na hivyo kuongeza uwezekano wa kujihusihsa na
ngono zisizotarajiwa na zisizo salama!
SASA KAZI KWAKO KUPAMBANUA!!!
HUU NI UTAFITI ULIOFANYWA NA MDAU WA GLOBU YA JAMII KUTOKA SUMBAWANGA
No comments:
Post a Comment