Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kutoka mji wa Indonesia wa Surabaya kwenda Singapore .
Imeelezwa kuwa mawasiliano ya mwisho na ndege hiyo iliyokuwa na mruko namba QZ8501 23:24 GMT.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 00:30 GMT.
Taarifa kutoka wizara ya uchukuzi inasema kwamba ndege hiyo ilipoteza mawasiliano wakati ikiwa bahari ya Javavya kati ya visiwa vya Kalimantan na Java .
Ofisa mmoja kutoka wizara hiyo Hadi Mustofa alisema ndege hiyo kabla ya kupoteza mawasiliano iliomba kibali kupita njia ambayo si ya kawaida na anga lilikuwa na mawingu sana.
No comments:
Post a Comment